Ni eneo ambalo lipo ndani/hatua chache kutoka Geita mjini lililoitwa eti!!! "Sophia Town"ambapo wakazi wake wanaishi kama wakimbizi ndani ya nchi yao,yaani walifukuzwa katika maeneo yaitwayo (Maini mpya)kumpisha Mwekezaji Ashanti(GGM) ambayo yalikuwa makazi yao.
Na sasa wanaishi katika mahema kwa muda wa miaka mnne sasa,na kwa taarifa tulizozipata wamesha poteza maisha watu takribani tisa (9)tangu walipo wasili eneo hilo......Baridi kali,njaa na magonjwa ya milipuko........Serikali na viongozi wao wametulia kama hawajui.
| Watoto wakiwa nje ya makazi yao mapya "SOPHIA TOWN" |
| Haya ndio makazi mapya... |
| Hapa ni ndani ya nyumba... |
| Watoto hawa wanacheza kwa furaha je! wategemee nini?Unadhani watoto hawa wana kesho inayo fananaje?Serikali Ogopeni basi hata dhambi..... |
| Baadhi ya waandishi wa habari wa TRJA wakijiandaa kikazi....huko Geita. |
| Ilibidi waingie ndani na kuanza kufanya kazi za kiuandishi.... |
| Baadhi ya waandishi TRJA wakiwa kazini huko Geita SOPHIA TOWN |
| Mtoto aliyezaliwa katika mahema hayo ya sophia town.....Mama wa mtoto akifanya mahojiano na Mwandishi wa TRJA. |
| Baadhi ya waandishi wa Habari TRJA Wakimwangali mtoto mchanga aliyezaliwa Ndani ya mahema SOPHIA TOWN huko Geita |
Tunaomba serikali ije huku Geita iwaokoe watu hawa.....Msichanganye Maisha ya watu na Siasa.

Post a Comment