Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha
Ualimu TABORA, Bwana PETER LABIA amesema kuwa walimu lazima wawe mfano wa
kuigwa katika jamii kutokana na kuwa na nidhamu na kufanya kazi yao kwa kutumia
busara zaidi.
Bwana LABIA alikuwa akizugumza katika
mahafali ya 58 ya Chuo cha Ualimu cha NDALA wilayani NZEGA ambapo aliwatunuku
vyeti wahitimu 465 wa mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti.
Akimkaribisha kutunuku vyeti kwa walimu hao
watarajiwa, Mkuu wa Chuo cha Ualimu NDALA, Bibi ALFRIDA ABEL amewahimiza
wahitimu kuwatii viogozi wa mamlaka watakazoenda kutumikia huku wakidumisha
amani, umoja na ushirikiano.
Kwa upande wao, wahitimu wa amfunzo ya ualimu
Chuo cha NDALA wameahidi kutoa elimu bora kwa wanafunzi kadri ya uwezo wao kwa
kuzingatia mafunzo waliyopata na kwamba watakuwa wapiganaji dhidi ya magonjwa
ya UKIMWI na malaria.


Post a Comment