CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI ZA VIJIJINI TANZANIA(TRJA) WATOA ZAWADI KWA WAANDISHI BORA...

Friday, December 9, 2011 | comments

Chama cha waandishi wa habari za vijijini Tanzania (TRJA) Cha toa zawadi kwa waandishi bora walioshiriki katika shindano lililofanyika tarehe 13 hadi tarehe 18 Mwezi wa 11 jijini Mwanza ndani ya Chuo Kikuu Cha Mtakatifu Augustino (SAUT) ambapo walishindanishwa zaidi wa waandishi 100 kutoka chuo hapo na hatimaye waandishi watatu wa kwanza walikabidhiwa zawadi katika BONANZA KUBWA LA KUADHIMISHA MIAKA 50 YA UHURUWA TANZANIA BARA LILILO FANYIKA KATIKA VIWANJA VYA MWANA KANENGE WILAYANI MISUNGWI JIJINI MWANZA,TAR 09.12.2011.

Akiongea katika Bonanza hilo Mwenyekiti wa asasi hiyo BW:ALEX MCHOMVU,alisema,muda umefika kwa waandishi wa Habari wa Tanzania kuungana na kuwatetea Wananchi wa vijijini ambao wao ndio asilimia kubwa ya Taifa letu.Ameongeza kusema kuandika Habari za vijijini ni kama Kujitoleo maana mazingira yake pia ni magumu na Hayamvutii Mwandishi kwenda.

Alimalizia kusema kuwa Wadau Mbalimbali,Serikali na Watu wenye mapenzi mema, wanaombwa kujitokeza kusaidia Asasi hii ya TANZANIA RURAL JOURNALISM kwani ipo kwaajili ya kila mtu kwa lengo la kuleta maendeleo kwa wananchi.

Mwenyekiti Wa TRJA Bw:Alex Mchomvu, akiongea na Wakazi wa misungwi jijini Mwanza.
Kulia ni Mkurugenzi wa Radio SAUT FM 96.1 Bw:DOTTO BULENDU EMMANUEL mwenye kofia nyeupe

Bonanza hilo ambalo lilitanguliwa na mashindano mbalimbali kama kufukuza kuku na mpra wa miguu lilimalizika na zawadi kukabidhiwa kwa washindi ambao washindi wa kwanza walipewa sh 20000laki mbili na wa pili laki moja na elfu thelethini 130000.
Vilevile zawadi zilitolewa kwa waashindi wa uandishi bora (TRJA)
Mshindi wa kwanza:Jacob Anthony. Zawadi ni Cheti cha kutambuliwa,Tisheti na Journal ya Africa Communication Research.
Mshindi wa Pili:Abdurahim Msonde.Zawadi ni Tisheti na Journal ya Africa Communication Research.
Mshindi wa Watatu:Denic Mtibulela.Zawadi ni Tisheti na Journal ya Africa Communication Research.
Wote kutoka katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino(SAUT)
Hizi ndizo zawadi walizo pewa washindi hao....
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Designer | Ibrahim Haruna | +255716606570
Copyright © 2011. SAUTI YA VIJIJINI - All Rights Reserved
Template Created by TheDynamite Published by TRJA
Proudly powered by Nativebase Company