Wanaoonekana pichani ni wanafunzi wa shule ya Msingi Juhudi iliyopo katika Wilaya ya Kigoma Vijijini mkoani Kigoma nchini Tanzania.
Mpiga picha hizi alikumbana na kizuizi na katazo kutoka kwa Walimu wa shule hiii pale alipokuwa akijiandaa kupiga picha hizi,inawaza mengi yanayoweza kuwa sababu ya kukatazwa kupiga picha, kubwa likiwa ni AIBU.
.Aibu kwa Walimu kufundisha katika mazingira haya hafifu kabisa.
.Aibu kwa Wanafunzi kupewa 'elimu' katika uduni huu wa mazingira ya kusomea.
.Aibu kwa uongozi na Bodi ya Shule.
.Aibu kwa uzembe wa Walimu, Wazazi, Wakuu wa Elimu tangu ngazi ya kata hadi Waziri wa Elimu.
.Aibu kwa Walimu, Wanafunzi, Wazazi na viongozi wa Elimu kutokudai mazingira stahiki ya Elimu.
.Aibu kwa Serikali kushindwa kutimiza ubora wa mazingira ya kuwapa elimu raia wake.
.Aibu kuwemo katika karne ya Sayansi na Teknolojia na ndani ya Taifa linalojisifu kupiga hatua ya kasi katika maendeleo huku sekta muhimu kabisa katika kulijenga na kulikuza Taifa - Elimu - likiwa nyuma kabisa.
TRJA inaamini kuwa ili Taifa liendelee, lazima mambo matatu yapewe kipaumbele cha pekee, nayo ni Elimu, Afya na Miundombinu ya kimawasiliano, mambo mengine yote yaliyobakia ni muhimu kama vile Kilimo, Biashara, Viwanda, Ulinzi nk lakini yoote haya yatakamilika vizuri zaidi ikiwa hayo makuu matatu yatatiliwa mkazo.
CHANZO :Upole Glog!


Post a Comment