Mageseni, kijiji cha Wamasai, Mkoka - Hongoro - Kibaigwa - Kongwa - Mpwapwa - Mlali - katika Mkoa wa Dodoma, vijiji hivi nilitembea sana katika kutatua shida ya maji, lakini bado shida hii inaendelea.
Nakumbuka sana na kupata hamu sana ya maisha yangu yaliyopita...enzi hizo za kuhangaika kusaka maji vijijini, ili kupunguza uhaba wa maji.....ambapo ukitembelea vijiji vingine mpaka machozi yanakutoka kabisa katika swala hili la maji na matatizo kibao yanayo wakabili wana Vijiji wengi Tanzania. Hizi picha nazitunza sana tena sana...kama mboni ya jicho langu ili kujikumbusha enzi hizo za kuhangaika huko vijijini...lakini kwa faida kubwa sana naamini hivi, maana watu walikuwa wakifurahi sana wakiona maji yanatoka....kwa wana vijiji wengi maji kwao ni dhahabu kabisa. Tunza maji...maji ni uhai.
Post a Comment