Mkuu wa Wilaya ya KARAGWE, DARRY RWEGASIRA amesema wanafunzi hao hawakujiunga na elimu ya
sekondari pamoja na kufaulu mtihani wa taifa katika kipindi hicho.
Pia amebainisha kuwa katika mwaka 2010
wanafunzi waliochaguliwa walikuwa 5,150 Kati ya hao 1,177 hawakuripoti shuleni huku mwaka 2011 wanafunzi 5,107 walichaguliwa na
2,155 hawakuripoti shule.
RWEGASIRA ameongeza kuwa katika mwaka 2012 kati ya wanafunzi 8,871
waliochagulia, wanafunzi 4,006 hawakuripoti shuleni.
Hata hivyo, amesema shule nyingi za sekondari
katika wilaya hiyo hazina miundombinu iliyodumu kutokana na baadhi ya wazazi
kutokuwa na mwamko wa kuchangia maendeleo ya shule.


Post a Comment