Tanzania Rural Journalism Association (TRJA) ya anzisha shindano la Uandishi ndani ya Chuo Kikuu Cha Mtakatifu Agustino (SAUT)

Thursday, November 17, 2011 | comments

TANGAZO!!! TANGAZO!!! TANGAZO!!!

Chama cha Waandishi wa Habari za vijijini Tanzania “TRJA”kimeanzisha shindano la kutafuta mwandishi bora kwa lengo la kujenga uwezo kwa Waandishi chipukizi ndani ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT)kupenda kuandika Habari za vijijini ambazo kwa kiasi kikubwa zimesaahuliwa na kuonekana hazina maana na Waandishi wengi wa Kitanzania.
Shindano hilo lilianza kushindaniwa tangu Tarehe 14/11/2011 hadi tarehe 18/11/2011 ambapo mshindi wa KWANZA,PILI na WATATU Wameahidiwa zawadi nono,ili kutoa motisha na kwa wengine kushiriki na Kupenda kuandika habari za vijijini.

MADA

JE! VYOMBO VYA HABARI VYA SASA VINACHANGIA KUKUZA MAENDELEO VIJIJINI?
AU,
JE! VYOMBO VYA HABARI VYA SASA VINACHANGIAJE KUZUIA ONGEZEKO LA WATOTO WA MITAANI TOKA VIJIJINI KWENDA MIJINI ?


MANENO YAWE KATI YA 500 HADI 700

TUMA KWENDA: sautivijijini@yahoo.com

Au peleka nakala yako iliyochapwa sehemu zifuatazo;
Stationary kwa Mama Herieth Nyamalango.(Kwa Mwl:Denis Mpagaze)
Capricon Stationary kwa Mwalimu Nkwabi.
Na kituo cha Redio SAUT FM Muone Mr. Maneno Sabini.

Mwisho wa kutuma kazi yako ni Tarehe 18/11/2011 saa nne Asubuhi.
Washindi watakabidhiwa Zawadi NONO na Mgeni Rasmi siku ya
“Black $ White Party.”(All Mass Communication Party)itakayo fanyika hivi karibuni.....

Kumbuka kuandika namba yako ya simu unapotuma kazi yako...

Kwa maelezo zaidi:
Tembelea: http//sautiyavijijini.blogspot.com au simu 0766238823/0784521755.

Mwote mnakaribishwa Kushiriki....Hatuta bagua Vitivo Kama unauwezo Tunahitaji Mchango/ushiriki wako.
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Designer | Ibrahim Haruna | +255716606570
Copyright © 2011. SAUTI YA VIJIJINI - All Rights Reserved
Template Created by TheDynamite Published by TRJA
Proudly powered by Nativebase Company