Naibu Waziri
wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mheshimiwa Adam Malima ametoa kauli hiyo bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Tabora
Kaskazini, Mheshimiwa Saffin Sumar
aliyetaka kujua serikali inawasaidiaje wakulima wa zao la tumbaku
kutokana na ufisadi mkubwa unaofanywa na chama kilele cha APEX na Chama kikuu
cha wakulima wa tumbaku kanda ya magharibi-WETCU kwa kuwaibia wakulima.
Naibu Waziri
amesema ubadhrifu na wizi wa fedha kwa wakulima wa tumbaku mkoa wa Tabora
ulitokana na viongozi wa WETCU kwa kushirikiana na baadhi ya watendaji
wasiokuwa waaminifu wakiwemo watumishi wa mabenki.
Amesema
katika kushughulikia tatizo hilo, serikali imeunda kamati maalumu chini ya
uenyekiti wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora ambayo pamoja na mambo mengine itakuwa na
jukumu la kuthamini madeni halali ya wakulima.

Post a Comment