Kutokana na
kukosa vitendea kazi sanjari na posho ndogo zinazolipwa wakati wa uendeshaji wa
kesi mbali mbali Mabaraza ya kata katika Halmashauri ya Manispaa ya Tabora yameshindwa kutekeleza
majukumu yake kwa ufanisi.
Katibu wa baraza la kata ya Mbugani Bwana Emmanuel Chambo amesema
suala la vitendea kazi kwa mabaraza ya kata limekuwa ni changamoto
inayokwamisha utendaji wa kazi zao.
Ameongeza kuwa
wamekuwa wakipokea kesi nyingi zinazowahusu wanandoa lakini wanashindwa
kuzitolea maamuzi sahihi kutokana na
kukosa ushahidi wa kutosha kwani matukio mengi yanakuwa ni ya siri baina yao
ndani ya chumba chao.
Bwana Chambo amefafanua kuwa ili haki ya mtu iweze kupatikana
ni vizuri vyema kuwa na ushahidi kwa sababu sheria inahusika zaidi panapokuwa
na ushahidi.
Amewataka wananchi kuhakikisha wanakuwa na ushahidi wa
kutosha wanapokwenda kufungua kesi katika baraza lolote la kata ili kutolewa
maamuzi yanayojitosheleza kwa mujibu wa sheria.

Post a Comment