Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina Lowassa wakiwasalimia wananchi wa kijiji cha Mswakini Wilayani Monduli walipowasili tayari kwa hafla fupi ya uzinduzi wa Vikoba katika kijiji hicho.
Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa akitoa hotuba yake kwa wananchi wa kijiji cha Mswakini Wilayani Monduli wakati wa hafla ya uzinduzi wa VIKOBA kijijini hapo. Lowassa katika hotuba yake, amesema kuwa ushirika wa VIKOBA ni sawa na mshipa wa damu kwa sera ya maisha bora kwa kila Mtanzania, pia alisema kuwa kutokana na kutambua hivyo ushirika wa Vikoba utaanzishwa katika wilaya nzima ya Monduli. Miasha bora kwa kila Mtanzania ni sera aliyoingia nayo madarakani Rais Jakaya Kikwete.
Post a Comment