APEWA TUZO LA UANDISHI BORA 'HABARI ZA VIJIJINI'

Saturday, January 5, 2013 | comments

MWANDISHI wa Habari wa Gazeti la Majira, Anneth Kagenda, amepewa tuzo ya uandishi bora wa habari za vijijini katika Wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani. Tuzo hiyo ilitolewa jana na mdau wa mazingira, Said Mswahili ‘Dk. Mswahili’ ambaye aliguswa na habari zilizokuwa zikilipotiwa na mwandishi huyo. Mswahili alisema waandishi habari wamezipa kisogo habari za vijijini, lakini mwandishi huyo ametumia muda mwingi kuelimisha wananchi juu ya utunzaji wa mazingira kwa wananchi wa Mkuranga. Alisema ataendelea kuandaa tuzo zaidi kila mwaka, ili kuwavutia waandishi kuandika habari za vijijini na hatimaye wananchi waweze kuelimika. Mswahili ambaye pia ni mganga wa tiba asili na mtabiri, alisema katika masuala aliyotabiri yameweza kutokea na mwandishi huyo aliripoti kama sehemu ya habari. Kwa upande wake, Anneth alishukuru kupata tuzo hiyo na kuwataka waandishi kuandika habari za vijijini kwa ajili ya kusaidia wananchi. Alisema ataendelea kuandika habari za vijijini si tu Mkuranga, bali atakwenda mbali zaidi kutokana na changamoto zinazowakabili wananchi katika maeneo hayo. Na Alex Mchomvu.
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Designer | Ibrahim Haruna | +255716606570
Copyright © 2011. SAUTI YA VIJIJINI - All Rights Reserved
Template Created by TheDynamite Published by TRJA
Proudly powered by Nativebase Company